Kamanda wa Polisi mkoa wa Dodoma Onesmo Lyanga, amesema jeshi la polisi mkoani humo linamshikilia dereva wa daladala ambaye jina lake limehifadhiwa kwa kosa la mauaji ya kondakta wa daladala Juma Hamis, wakati wakigombea abiria.
Akizungumza na wandishi wa habari leo Julai Mosi, 2021, Kamanda Onesmo amesema kuwa mtuhumiwa huyo alitenda kosa hilo Juni 15 mwaka huu katika mtaa wa Mji Mpya Jijini Dodoma ambapo alimuuwa kwa kumpiga na jiwe kichwani wakati wakigombea abiria kwenye eneo hilo.
Kamanda Lyanga ameongeza kuwa dereva huyo mara baada ya kuona abiria walianza kugombea na marehemu huku kila mmoja akitaka abiria aingie kwenye gari yake.
Kamanda Lyanga amesema mara baada ya msako kufanyika Juni 19 mwaka huu, wamefanikiwa kumkamata dereva huyo akiwa mafichoni katika Kijiji cha Galapo wilayani Babati mkoa wa Manyara na kusema kuwa mtuhumiwa anatarajiwa kufikishwa Mahakamani kwa kosa la mauaji.
Post a Comment