Polisi "Bastola aliyokua nayo Marehemu Alex Korosso ilikua ni Bastola Anayoimiliki Kihalali"




Polisi Kinondoni Dar es salaam wamesema Bastola aliyokua nayo Marehemu Alex Korosso na kuitumia kumpiga Gift Mushi na kumsababishia kifo kabla na yeye kujipiga na kufariki, ilikua ni Bastola anayoimiliki kihalali.

"Alex alikua anamiliki silaha hiyo kihalali tunaendelea kufatilia uhalali wake lakini pia njia alizozifuata kuipata kama zilikua sahihi, vilevile tunapoona Watu wame-behave kama tulivyomuona Alex msiache kutoa taarifa ya tabia hizi za Watu wanaotumia silaha hata kama wamezipata kihalali, mkitoa taarifa mapema tunaweza kuzuia matukio kama haya”

Kwenye upande mwingine Kamanda wa Polisi Mkoa wa Kipolisi Kinondoni Ramadhani Kingai amesema Watanzania wanatakiwa kutoa taarifa kituo cha Polisi haraka iwezekanavyo pale wanapoona Mtu anatishia wengine kwa Bastola popote pale.

"Nitoe wito kwa Wananchi si vyema kwenda kwenye Baa na sehemu za starehe ukiwa na silaha sababu ukiwa umeshakunywa pombe akili inakua haiko sawasawa, unaweza kuwa na maamuzi ya haraka mfano Mtu akakutukana au maongezi ya kawaida tu ukayaona ni jambo la kuchukiza na ukatumia silaha" ——— Kamanda  Ramadhani Kingai. …RIP GIFT MUSHI  


0 Comments

Post a Comment

Post a Comment (0)

Previous Post Next Post