Picha na Kauli ya Rais Samia Wakati Akichoma Chanjo

 


Rais wa Tanzania Samia Suluhu Hassan, leo Julai 28, 2021, amechoma chanjo Johnson & Johnson inayotolewa kwa dozi moja tu, ili kujikinga na maambukizi ya virusi vya Corona ambapo amesema kuwa amefanya hivyo kwa hiari yake mwenyewe baada ya wanasayansi kujiridhisha na usalama wa chanjo hiyo.


“Mimi ni mama wa watoto 4 na ni bibi wa wajukuu kadhaa wanaonitegemea,ni mke pia, ni rais na amri jeshi mkuu..nisingetoka kujihatarisha wakati ninategemewa. Sioni hatari iliyopo kuchanjwa. Wanasayansi wamejiridhisha na Mimi nipo Tayari kuchanjwa” Samia Suluhu Hassan

Kauli hiyo ameisema leo Ikulu ya Dar es Salaam, ambapo amesisitiza kwamba yeye ni Mama, Rais na Amiri Jeshi Mkuu wa Majeshi ya Tanzania, Bibi na mke pia, hivyo asingejipeleka mwenyewe kwenye kifo licha ya kuwa na majukumu mengi kwenye Taifa.



0 Comments

Post a Comment

Post a Comment (0)

Previous Post Next Post