Paula Anaweza Kuwa Msichana Mwenye Mafanikio Mpaka Dunia ikashangaa

 


Nimeona mitandao ikimbeza sana Supastaa wetu mpya wa kike Tanzania mtoto wa Kajala aitwae Paula.

Wengi wanamchukulia Paula kama mtoto wa kike aliyeshindikana na amepoteza uelekeo wa maisha.

Wengine sababu ya elimu sababu hakufanya vizuri darasani. Na kuna wanafki wanasema kaanza mapenzi akiwa mdogo.

Mimi nataka niwaambie endapo Paula akisimamiwa vizuri na akaitumia mitandao kama sehemu ya kupiga hela basi atakuwa na pesa nyingi mpaka watu washangae.

Anachohitaji sasa hivi ni kupata management nzuri na branding nzuri.

Habari za Paula zinafatiliwa kuliko sociolite yoyote wa kike kwa hapa bongo sasa hivi. Huu ni mtaji mkubwa sana kwake kuliko hivyo veti mnavyoona ndio dili. Kazi ni kwake kubadili kelele za mitandao kuwa pesa atajenga ataendesha gari analotaka na anaweza kuwa na biashara kubwa tu akiwa na umri mdogo.

Watu wa showbiz nafikiri watanielewa zaidi.



0 Comments

Post a Comment

Post a Comment (0)

Previous Post Next Post