Jeshi la Polisi mkoani Mwanza linawashikilia watu 128, akiwemo Askofu Emmaus Mwamakula, Dkt. Lwaitama pamoja na baadhi ya viongozi wa kitaifa, mkoa na wilaya wa CHADEMA wakati wakijiandaa kuhudhuria kongamano la kudai Katiba Mpya.
Mkutano huo ulitarajiwa kufanyika leo, Julai 17, 2021 katika Hoteli ya Boma, Nyakato jijini Mwanza lakini siku moja kabla ya kufanyika, Jeshi la Polisi lilimuandikia barua Katibu wa Vijana wa Chadema, Wilaya ya Ilemela na kumtaarifu kwamba hawakuwa wametoa taarifa wala kupata kibali cha kufanya kongamano hilo.
Katika barua hiyo iliyosainiwa na Kamanda wa Polisi Wilaya ya Ilemela, ASP Shamila Mkomwa, ilieleza kwamba kwa kuwa Chadema hawakuwa wameomba kibali wala kuruhusiwa, kwa mujibu wa sheria, kongamano hilo ni batili na limepigwa marufuku.
Hata hivyo, licha ya zuio hilo kutoka kwa Jeshi la Polisi, wafuasi na viongozi wa Chadema, walikusanyika katika hoteli hiyo, hali iliyosababisha Jeshi la Polisi kuingilia kati na kuwakamata baadhi yao.
Post a Comment