Mwanariadha wa Marekani Aenguliwa Katika Mashindano ya Olimpiki Baada ya Kukutwa Anatumia Bangi


Mwanariadha wa Marekani Sha'Caari Richardson ameenguliwa kushiriki mbio za Mita 100 kwenye michuano ya Olimpiki 2020 ambayo itaanza Julai 23 mwaka huu Tokyo nchini Japan. Sababu zilizopelekea mwanadada huyo kuenguliwa ni baada ya kufanyiwa vipimo na kubainika kuwa anatumia bangi.

Mamlaka inayohusika kuzuia dawa zisizoruhusiwa michezoni nchini Marekani imetangaza matokeo hayo leo Ijumaa ikiwemo kumfungia kwa kipindi cha mwezi mmoja, hukumu ambayo imeanza Juni 28 mwaka huu. Kwenye mahojiano na NBC, Richardson (21) amesema aliamua kutumia bangi ili kuondoa mawazo baada ya Kifo cha mama yake mzazi. Watu mbali mbali wametoa maoni yao kuhusu hili na kuliweka kwenye mlengo wa uonevu na ubaguzi. Kupitia ukurasa wake wa twitter ameandika maneno mawili tu "I am Human." .

Mwanadada Gabrielle Union amesema;

"Bangi ni nzuri kwa vitu vingi lakini kukimbia kwa haraka sio miongoni mwa vitu hivyo. Muacheni akimbie." ilisomeka tweet yake.




0 Comments

Post a Comment

Post a Comment (0)

Previous Post Next Post