Mwanamuziki Spack Afunguka Kuhusu Kurogwa na Kutapeliwa

 


Msanii na hitmaker wa ngoma ya 'nipe ripoti' aliyofanya na Captain Tundaman, Spack Tz amefunguka ukweli kuhusu stori zilizokuwa zinasemekana kwamba amerogwa na ametapeliwa kwenye muziki.

Spack amesema kuna maneno mengi yamezungumzwa kuhusiana na yeye kipindi ambacho amekaa kimya kwa muda mrefu ila binafsi hajawahi kukaa na jambo  rohoni mwake.

"Kuna maneno na mambo mengi yamekuwa yakiendelea lakini binafsi sijawahi kuweka kitu katika roho na kama kuna vitu vingine nyuma sikuvijua, maneno hayo nimeyasikia ila sijamuona wa kumuhukumu" 

"Binaadam wa kawaida hana nguvu ya kustopisha yanayoendelea kwamba nisisemwe, kama kuna mtu anasema nimerogwa ni yeye atajua mwenyewe yote kwa yote najijua kama nipo" ameeleza msanii Spack 



0 Comments

Post a Comment

Post a Comment (0)

Previous Post Next Post