Mwanaume aliyefahamika kwa jina moja la Khamisi maarufu (Zungu), amefariki dunia baada ya mpenzi wake Neema Mushi waliokuwa wanaishi naye Mbezi Makabe jijini Dar es Salaam, kuchoma moto nyumba hiyo na kusababisha kifo kwa kile kinachodaiwa wamepishana kauli, huku fremu za wafanyabiashara zilizokuwa kwenye nyumba hiyo kuteketea moto.
Kwa Mujibu wa Mwandishi wetu Juma Kapalatu aliyefika kwenye nyumba hiyo ambayo kijana huyo alikuwa anaishi na mpenzi wake, ametueleza kuwa nyumba hiyo mmiliki mkubwa ni Neema ambaye alikuwa akiishi na bwana Khamisi, ambapo jeshi la polisi limefika na kuchukua mwili wa kijana huyo.
Post a Comment