Baada ya klabu yake ya Wydad Athletic Club Jumatano hii ya Julai 28,2021 kutwaa ubingwa wa ligi kuu ya Morocco ‘Botola Pro League’, Simon Msuva ana kuwa mwanasoka wa tatu wa Wakitanzania kufanikiwa kutwaa ndoo nje ya nchi kwa karne ya 21.
Tangu wachezaji wa kitanzania walipoanza kuchangamkia fursa ya kucheza soka la kulipwa Mbwana Samatta, Thomas Ulimwengu na Simon Msuva wote kwa pamoja wamefanikiwa kutwaa jumla ya mataji 12 ya ligi kuu na timu zao.
Ulimwengu ametwaa makombe 6 ya ligi (League 1) akiwa na Tp Mazembe ya DR Congo, 1 akiwa na Al-Hilal Club ya Sudan, huku Samatta akiwa na ndoo 4 za League 1 akiwa na klabu yake ya zamani Tp Mazembe, na 1 akiwa na KRC Genk inayoshiriki First Division A huko Ubelgiji katika msimu wa 2018/2019.
Huku Jalai 28 Msuva nae ameandika historia ya kuvaa medali ya ubingwa wa Ligi Kuu ya Morocco ‘Botola Pro League’ baada ya timu yake ya Wydad Athletic Club kutwa ubingwa wa msimu huu wa 2020/21.
Post a Comment