Msanii Zuchu Afunguka Kuingiza MILIONI 10 za Kitanzania Kupitia Youtube Ndani ya Mwezi Mmoja

 


Nyota wa muziki wa kizazi kipya msanii @officialzuchu amefunguka kwa mara ya kwanza juu ya hili, ndani ya mwezi mmoja kupitia channel yake ya YouTube aliweza kuingiza Euro 4000 ambazo ni takribani MILIONI 10 za Kitanzania.

#Zuchu amefunguka hayo mapema wiki hii wakati anaongea kwenye semina ya Wasanii wa Zanzibar ambayo ililenga mafunzo maalum kwa wasanii juu ya kukuza vipaji vyao, pamoja na kutumia sanaa zao kujinufaisha kibiashara.

Hit maker huyo wa "Nyumba Ndogo" amesema katika moja ya mafanikio ambayo hakuwahi kuyadhania awali ni kutengeneza fedha katika mitandao ya kijamii kupitia sanaa yake ya muziki. Akitolea mfano; amesema kwa mara ya kwanza anapigiwa simu na Boss wake kwamba amewekewa kwenye akaunti yake kiasi cha fedha ‘Euro 4,000’  pesa iliyopatikana kupitia kazi zake YouTube.. hakuamini.

“Kipindi natoa Zuchu Ep nikapigiwa simu hela yangu ya youtube imeingia, kipindi hicho nilikuwa sijui sana mambo ya Euro inachenjiwa vipi, niliambiwa nimewekewa euro 4,000 kwenye akaunti yangu kupitia akaunti ya youtube nikasema aaah hizo zitakuwa ni hela ndogo tu"

“Siku moja nikasema ngoja nipite benki, nikauliza euro 4,000 ni shilingi ngapi nikaambiwa ni kama Sh10 milioni nilishangaa sana. Nikaanza kupiga simu mara mbili mbili hiyo ni pesa yangu ya mwezi mmoja siamini, hivyo msishangae ukiona mtu anashangilia kupata watazamaji milioni moja YouTube ujue anashangilia pesa,” amesema Zuchu.

Fahamu kuwa @officialzuchu katika channel yake ya Youtube ana wafusi (subscribers) MILLIONI 1.43 akiwa msanii wakike wa kwanza Tanzania kuwa na wafuasi wengi katika mtandao huo. Pia channel hiyo imefikisha watu milioni 200 (Total Views) waliotazama kazi zake mbalimbali ikiwa ni mwaka mmoja na miezi yake kadhaa tangu aingie rasmi kwenye muziki.



0 Comments

Post a Comment

Post a Comment (0)

Previous Post Next Post