Msanii wa Muziki wa Mduara AT Amewataka Wazanzibar Wamsupport Harmonize na Wasidanganyike na Upande wa Pili



Kupitia ukurasa wake hiki ndicho alichokiandika 👇👇👇
"Nimekuwa nikifanya kazi kwa Kuzingatia Ukubwa wako na Heshima ya Watu wetu wote Nichukue nafasi hii kukushukuru wewe @harmonize_tz na kila shabiki wako na Uwongozi Mzima Kwa kufanya Leo AT azungumzike atizamike Upya pamoja na kuwashukuru kwa Dhati Media's Zote kwa kila sekta na Fans wangu na Wasanii wenzangu wote wanaonipenda na wasionipenda mimi niseme Shukran sana sana Mubarikiwe Naomba nitoe Ahadi ya kufanya Kazi Nzuri zaidi na kwa uadilifu.
Wazanzibar Naomba Niwaambie Tu Huyu Kijana Ni ndugu yetu anaroho ya kipekee Tokea nimekuwa nae karibu na Kuna Makubwa kwa Bara na Visiwani kwetu Get ready msirubuniwe Njooni nilipo Nasema CHECHEI kila Mmoja aitikie CHECHEI Tusonge mbele🙏🙏 #X👑"
.
.
.
.
MAONI YANGU:
Sijajua ni kiasi gani jamaa ana ushawishi huko Zanzibar ila hii kauli sio ya kisanii 😂😂😂Haya mambo ndio yanawapoteza wasanii wa zamani, huwa wanaingia kwenye vita bila kujiuliza. Zamani AT alikuwa Team Kiba kindakindaki sijajua imekuwaje kahamia kwa Harmonize 😂😂, kumchukia Diamond huku unasaidiwa na aliyesaidiwa na Diamond ni sawa na kumtukana Mama mkwe madhara yake makubwa sana.
Wazanzibar wanapaswa kujiuliza kwasasa kati ya AT na ZUCHU nani anawakilisha Zanzibar?? Je, AT anaweza kusimama tena kimuziki kama zamani kama H. BABA ana miaka miwili kashindwa yeye ataweza ikiwa Cheedy hajatambulishwa na ANJELLA bado hajaeleweka mtaani??
Elimu ya Bure kwa wasanii wa Zamani, jamani nyie bado mnapendwa sana hamna sababu ya kuwa Chawa ili mutoboe, hamna sababu ya kujihusisha na vita za wasanii ili mufanikiwe. Andaa show zako pangilia kusanya hata ikiwa Laki 3, ukifanya chaka to Chaka mwezi mmoja hukosi Milioni 5, ukifanya hivyo mwaka kwa Malengo Milioni 50 unapata, then unajianda upya kufanya uwekezaji mkubwa wa kurudi kwenye Game. Niwape Siri moja Hakuna msanii anapendwa Mikoani kama Nay wa Mitego, na Nay ana akili kubwa sana. Anachofanya Nay anaamsha Goma kali, likishatikisa anaingia mikoani anakusanya hela zake safi maisha yanaendelea. Nay ni Mfanyabiashara mzuri wa muziki


0 Comments

Post a Comment

Post a Comment (0)

Previous Post Next Post