Kiungo mshambuliaji Bernard Morrison, amechaguliwa Mchezaji Bora wa Mashabiki wa Mwezi Juni (Emirate Aluminium Simba Fans Player of the Month).
Morrison raia wa Ghana amewashinda nyota wawili Nahodha John Bocco na Luis Miqiussone ambao aliingia nao fainali ya kinyan’ganyiro hicho.
Mchakato wa tuzo hiyo unahusisha mashabiki ambao ndiyo wenye dhamana ya kupiga kura kupitia tovuti rasmi ya klabu baada ya Kamati Maalumu kuchuja majina matatu kutoka matano ya awali.
Moja ya tukio kubwa alilofanya Morrison katika mwezi huo ni lile la kuanzisha mpira kwa haraka na kutoa pasi iliyozaa bao lililofungwa na Miqiussone na kutupeleka fainali ya Azam Sports Federation Cup katika Uwanja Majimaji, Juni 26 mwaka huu.
Morrison atakabidhiwa kitita cha Sh 1,000,000 kutoka kwa wadhamini Emirate Aluminium Profile ambao walianza kutoa tuzo hiyo tangu Februari mwaka huu.
Mchanganuo wa kura
Idadi ya kura zilizopigwa 9,356
Morrison amepata kura 6,697 sawa na asilimia 72
Luis amepata kura 1,978 sawa na asilimia 21,
Bocco kura 681 sawa na asilimia saba.
MZEE WA UTOPOLO AWAKA KUELEKEA DERBY, AMLIPUA MANARA “ANABWABWAJA TU “
Post a Comment