Morrison Aondolewa Kikosini Simba




KIUNGO Mshambuliaji wa Simba, Bernard Morrison, ameondolewa kwenye kikosi cha timu hiyo kufuatia kuwa na matatizo ya kifamilia.

 

Morrison ambaye wikiendi iliyopita kwenye mchezo wa Ligi Kuu Bara dhidi ya Yanga ambao Simba walifungwa bao 1-0 alicheza dakika zote tisini, anatarajiwa kuukosa mch–ezo wa leo Jumapili dhidi ya Coastal Union utakaochezwa Uwanja wa Mkapa, Dar.

 

Katika mazoezi ya jana Jumamosi yaliyofanyika Simba Mo Arena, Dar, na kushuhudiwa na Spoti Xtra, Morrison hakuwa sehemu ya mazoezi hayo ya mwisho kabla ya kuivaa Coastal Un–ion leo Jumapili.

 

Meneja wa Simba, Patrick Rweyemamu, alisema: “Morrison hayupo na timu kwa sababu ya matatizo ya kifamilia, pia kuna wachezaji wengine watakosekana katika mchezo dhidi ya Coastal akiwemo Parfect Chikwende ambaye yupo na kikosi cha timu yao ya taifa.”

STORI: CAREEN OSCAR,Dar es Salaam



0 Comments

Post a Comment

Post a Comment (0)

Previous Post Next Post