AMKENI…amkeni…! Unaambiwa huko nchini Afrika Kusini kumenoga kufuatia mahaba mazito ambayo yapo fulu chaji kati ya Msanii wa Bongofleva, Diamond Platnumz na mzazi mwenzie, Zarina Hassan ‘Zari the boss lady’.
Miongoni mwa mambo ambayo yamewapa furaha kupita kiasi wafuasi wa Zari na Mondi ambao ni zaidi ya milioni 20 kwenye Mtandao wa Instagram, ni kitendo cha wawili hao kuonekana kwa mara nyingine wakifurahiana.
Habari za ndani zinasema kuwa, zamani Mondi alipokuwa anakwenda nchini Afrika Kusini alikuwa anafikia kwenye apartment, lakini sasa hivi anaongoza njia moja kwa zote hadi nyumbani kwa Zari.
Hata hivyo, Zari amekuwa akiweka ngumu kukubali kwamba amerudiana na Mondi kwa maelezo kwamba ukaribu wao unatokana na malezi ya watoto wao wawili, @princess_tiffah na @ princenillan.
Hii ni mara ya pili Mondi kurejea Afrika kusini kwani ndani ya kipindi cha miezi mitatu hivyo kuzidisha ukaribu wake na Zari ambao mashabiki wamekuwa wakifurahia wawili hao kurudiana.
Post a Comment