Mfahamu Dereva wa Basi Anayetrend Mitandaoni Kila Kona




Dar es Salaam. Dereva wa ‘Ndugu Abiria’ ambaye ana-trend kwenye mitandao ya kijami amezungumzia picha zake zinazozunguka kwenye mitandao na kuwekwa maelekezo mbalimbali zilivyomsumbua na kumchekesha.


Picha za Waubani Linyama ambaye ni dereva wa kampuni ya New Force ambaye anaendesha basi linalofanya safari za Dar es Salaam- Tunduma mkoani Songwe zimekuwa zikisambaa kwenye mitandao ya kijamii na zikiambatanishwa na baadhi ya maneno mbalimbali.


Mwananchi Digital iliamua kumtafuta dereva huyo kwa mahojiano maalum ili aeleze anazionaje na kujisikiaje watu wanavyoweka maneno kwenye picha yake, linyama amesema picha hizo zilipigwa miaka minne iliyopita na dereva mwenzake.


Picha hizo ambayo zinamuonyesha Linyama akiwa kwenye usukani ameshikilia kipaza sauti zimekuwa zikiambatanishwa na maneno mbalimbali.



Amesema kuwa “Picha ile aliipiga na dereva mwenzangu Faraji Kindole na kuiweka status ya simu yake na kuna mtu nahisi aliichukua, kwa sababu ni picha ya muda mrefu ina miaka mine,” amesema.


Amesema hawezi kujua sababu za picha hiyo kusambaa sana lakini na yeye anakutana nazo sana kwenye mitandao ya kijamii.
Hata hivyo, anaeleza kuwa picha hiyo ilikuwa wakati wakiwa safarini, wanaingia hotelini Mafinga kwa ajili ya kupata chakula na kuchimba dawa.


Amesema siku hiyo kweli alitamka maneno ambayo yanaendana na yanayoambatanishwa na picha kwa sasa kama nukuu inayosema hapo chini.



“Tulikuwa tumeingia hotelini Mafinga, nikawa nawatangazia. Ndugu abiria tunaingia hotelini kwaajili ya kupata chakula cha mchana na kuchimba dawa dakika kumi, tafadhali tuzingatie muda na tukitoka hapo kituo kinachofuatia ni mkoa wa Morogoro,” anaeleza dereva huyo.


Maneno yanayoambatanishwa na picha zake.
Ameeleza kuwa hakutegemea kuwa picha hiyo itasambaa kwa kipindi hiki japo anaeleza kuwa wakati mwingine zinamfurahisha.


Pamoja na kukiri kuwa picha hizo zikiambatanishwa na maneno zinachekesha lakini anasema kuwa maneno mengine yanaleta tafrani.


“Inachoniumiza zaidi juzi wanasemaa mapenzi yamenichanganya natamani nife, ile imeleta kidogo changamoto,” ameeleza akirejea picha ambayo ilikuwa inasambaa ikiwa imeambatanishwa na maneno kuwa “Ndugu Abiria najua haiwahusu lakini mapenzi yananitesa natamani nife.”



Amesema kuwa anatambua kuwa mapenzi yakimchanganya mtu hawezi kufanya kazi ila kwake hayajamchanganya.
“Hilo limenichanganya maana hata wife akiona anaweza akafikiri kuna mchepuko umenichanganya kumbe sio,” amasema Wanyama ambaye ni baba wa familia.


Anasema kuwa hata mke wake baada ya kuona picha hiyo ya mapenzi yananitesa, alimuulizi kama kuna mtu ambaye yuko kwenye mahusiano naye anamtesa.


“Ile inayosema mapenzi yananichanganya natamani nife, alijaribu kuniulizia ni nani ananichanganya, lakini kwa vile ni muelewa alinielewa.”


Akizungumzia picha ambayo imemfurahisha amesema kuwa ni ile ambayo anaonekana amelala ikiwa imeambatanishwa na maneno.

Nafasi za Ajira Serikalini Bonyeza HAPA

Nafasi za Scholarships Bonyeza HAPA

“Abiria mimi sijalala niko njiani nafikiria kwenda kuwarusha kwenye matuta ya Igawa, lile ndio limenichekesha saana,” anasema.

dereva pc 3

Amesema kuwa pamoja na kwamba zinachekesha lakini zile ambazo zinaandikwa “Gari limefeli breki nawatumbukiza mtaroni hilo sio zuri,” anaeleza Linyama ambaye amekuwa anaendesha mabasi ya mikoani kwa zaidi ya miaka 18 sasa.


0 Comments

Post a Comment

Post a Comment (0)

Previous Post Next Post