Kumetokea kituko kortini mjini Eldoret nchini Kenya baada ya mtuhumiwa Wilberforce Manyongemwenye umri wa miaka 28 aliyeshtakiwa kwa kukutwa na misokoto 50 ya bangi kusema kwamba yeye huvuta ili kufukuza mapepo kutokana na kazi yake ya kuchimba makaburi eneo la Kiplombe.
Mshukiwa, Wilberforce Manyonge, alikiri kosa hilo la kupatikana na misokoto 50 ya bangi yenye thamani ya KSh 2,500 sawa na shilingi 52,000 za Tanzania.
Kupatikana akiwa na bangi Korti iliambiwa kwamba Jumatatu, Julai 5, 2021, Manyonge alipatikana akiwa na bangi katika eneo la Kituo cha Reli cha Eldoret ndani ya kaunti ndogo ya Soy huko Uasin Gishu.
Alipokuwa mbele ya Hakimu Mkazi Mwandamizi wa Eldoret Barnabas Kiptoo, alikanusha kuwa mfanyabiashara wa dawa za kulevya, akisema kwamba bangi ambayo ilipatikana kwake ilikuwa ni kwa ajili ya matumizi yake binafsi kwani "humpa nguvu" kuchimba makaburi kwenye makaburi maarufu ya Kiplombe kwenye viunga vya mji wa Eldoret.
Aliiambia korti kuwa kwa sababu ya aina ya kazi yake, ambayo ni pamoja na kuchimba makaburi na wakati mwingine kufukua mifupa ya binadamu, yeye hupata ndoto mbaya za kutisha, kwa hiyo ili kufurahia usingizi wake, analazimika kutumia bangi kuondoa uoga na kufukuza mapepo.
Manyonge ambaye alikamatwa na maafisa wa polisi akiwa doria alisema kuwa haoni ubaya wowote wa kuvuta bangi ambayo kwake ni dawa na chanzo cha nguvu.
"Ni kweli kwamba nilikamatwa na misokoto 50 ya bangi. Haikuwa ya kuuza lakini ni dawa yangu mwenyewe. Kama mchimbaji wa kaburi, mimi huvuta bangi kuzuia ndoto za jinamizi na uoga kutokana na hali ya kazi yangu,” mtuhumiwa aliiambia korti wakati wa kesi.
Post a Comment