Baadhi ya wanafamilia ya Rais wa zamani wa Zambia Kenneth Kaunda wamekwenda kortini kujaribu kuzuia mazishi yake katika uwanja wa kitaifa wa Embassy Park katika mji mkuu Lusaka.
Kaunda – rais wa kwanza wa nchi hiyo ambaye alikuwa afisini kutoka 1964 hadi 1991 – aliaga dunia mnamo 17 Juni akiwa na umri wa miaka 97.
Serikali baadaye iliamuru kwamba atazikwa katika eneo la Embassy Park ambapo marais wengine wa zamani wamelazwa. Mazishi hayo yanapaswa kufanyika siku ya Jumatano.
Lakini sasa baadhi ya watoto, wajukuu na vitukuu wa Kaunda wanaomba korti iruhusu kiongozi huyo wa zamani kuzikwa mahali pengine, karibu na mkewe Mama Betty Mutinkhe Kaunda.
Wanasema hii itakuwa kulingana na matakwa yake ya mwisho.
Haijulikani ni wangapi katika familia ya Kaunda wanaounga mkono msimamo huu na ikiwa mazishi yataahirishwa sasa.
Serikali ya Zambia haijatoa tamko juu ya suala hilo
Post a Comment