Mastaa Wapumzishwa Simba SC Kisa Yanga SC





IMEFAHAMIKA kwamba mpango namba moja wa Kocha Mkuu wa Simba, Didier Gomes kuwapumzisha mastaa wake ikiwa ni pamoja na Luis Miquissone, Clatous Chama ni kwa ajili ya fainali dhidi ya Yanga.

 

Mchezo huo unatarajiwa kuchezwa Julai 25, Uwanja wa Lake Tanganyika Kigoma unatarajiwa kuwa na ushindani mkubwa kwa kuwa Simba ni mabingwa watetezi wa taji hilo wanakutana na watani zao wa jadi Yanga ambao wamebainisha kwamba wanalihitaji kombe hilo.

 

Taarifa kutoka benchi la ufundi la Simba zimeeleza kuwa mbali na kwamba kwa sasa walikuwa wanawapa nafasi wachezaji ambao walikuwa hawapati nafasi kikosi cha kwanza ila hesabu kubwa ni kwa ajili ya mchezo dhidi ya Yanga.

 

“Tuna jambo kubwa la kufanya kuelekea mchezo wetu dhidi ya Yanga hivyo tuliamua kuwapa mapumziko wachezaji wetu wale ambao walicheza mechi nyingi, moja kuwapa nafasi wale wengine pamoja na kuwapa muda wa kujiandaa na mchezo wetu dhidi ya Yanga,” ilieleza taarifa hiyo.

 

Kocha Mkuu wa Simba, Didier Gomes aliliambia Championi Jumatatu kuwa wanatakiwa kutwaa taji la Shirikisho na mbinu pekee ni kushinda mbele ya Yanga.

 

Rekodi zinaonyesha kuwa Julai 15, wakati ubao wa Uwanja wa Azam Complex ukisoma Azam FC 1-1 Simba, Aishi Manula kipa namba moja kinara wa clean sheet akiwa nazo 17, Shomari Kapombe beki wa pembeni, Mohamed Hussein, nahodha msaidizi, Pascal Wawa beki wa kati, Taddeo Lwanga mzee wa kukata umeme pamoja na Clatous Chama kinara wa pasi za mwisho akiwa nazo 15 hawakuanza kikosi cha kwanza.

 

Pia wakati Simba ikitangazwa kuwa mabingwa Julai 11 kwa ushindi wa mabao 2-0 dhidi ya Coastal Union ni Manula, Kapombe,Mohamed, Joash Onyango,Wawa, Lwanga, Kagere na Kapombe hawakuanza kikosi cha kwanza.

Lunyamadzo Mlyuka, Dar es Salaam.



0 Comments

Post a Comment

Post a Comment (0)

Previous Post Next Post