Maskini.. Ndugu Aeleza Kauli ya Mwisho ya Anna Mghwira



Arusha. Ndugu wa aliyekuwa Mkuu wa Mkoa Kilimanjaro, Anna Mghwira ambaye alifariki dunia jana katika Hospitali ya Mkoa ya Mount Meru wameeleza kauli zake za mwisho kabla ya kufariki.


Akizungumza na Mwananchi, mdogo marehemu Anna Mghwira, Hellen Mghwira ambaye alikuwa akimuuguza Hospitali ya Mount Meru amesema jana asubuhi kabla ya kufariki, alikuwa anasema amechoka kutumia mashine za hewa ya Oksijeni.


Hellen amesema dada yake alisema anaendelea vizuri na akitaka kurejeshwa nyumbani akatumie dawa za asili na hospitali.

“Baadaye alizidiwa na kurejeshwa chumba cha wagonjwa mahututi (ICU) na muda mfupi alifariki duniani," amesema Hellen.
Daniel Mghwira ambaye naye ni mdogo wa marehemu amesema dada yake alianza kuumwa tangu Jumatano na ilielezwa anaumwa nimonia kali na alianza kutibiwa Hospitali ya Nkoaranga.


Amesema baadaye walimhamishia Hospitali ya Rufaa ya Mkoa Arusha ya Mount Meru ambapo umauti ulimkuta.

Baadhi ya majirani wa Mghwira ambaye anaishi eneo la Manyata mji mdogo wa Usa River wanamueleza Mghwira kama kiongozi aliyependa watu na hakuwahi kutambia madaraka.
Jeremiah Silayo anasema Mghwira atakumbukwa kama kiongozi ambaye hakuwa na makuu alipenda watu wote alishiriki katika shughuli mbalimbali za kijamii bila kujali nafasi yake.
"Licha ya kuwahi kugombea urais na kuwa Mkuu wa Mkoa Kilimanjaro aliporejea nyumbani alikuwa mtu wa kawaida alishiriki shughuli mbalimbali za kijamii," amesema.

Godluck Peter anasema licha ya kuwa jirani Mghwira aliwahi kumfundisha katika makongamano ya ujasiriamali ambayo alipenda kutoa elimu kwa vijana na wanawake kujikwamua na umaskini.
Taratibu za mazishi zinatarajiwa kutolewa leo. Endelea kufuatilia Mwananchi


0 Comments

Post a Comment

Post a Comment (0)

Previous Post Next Post