Mashahidi wa kesi namba 66 ya jinai ya mwaka 2021 wanatarajiwa kutoa ushahidi katika mashtaka mawili ya unyang’anyi kwa kutumia silaha, yanayomkabili aliyekuwa mkuu wa wilaya ya Hai mkoani Kilimanjaro, Lengai Ole Sabaya na wenzake watano leo, Ijumaa, Julai 16, 2021.
Sabaya na wenzake watano wamepandishwa kizimbani katika Mahakama ya Hakimu Mkazi mkoani Arusha leo kwa mara ya nne wakikabiliwa na mashtaka matano ya uhujumu uchumi, rushwa, kuongoza genge la uhalifu, utakatishaji wa fedha na unyang’anyi wa kutumia silaha.
Mbali na Ole Sabaya, washtakiwa wengine ni msaidizi wake wa karibu, Silvester Stanslaus, Enock Togolani, John Odemba, Daniel Gabriel, na Waston Mwakomange.
Post a Comment