Baada ya Kipigo kitakatifu alichopokea Simba Kutoka Kwa Yanga, Mange Kimambi Ameibuka na Kufunguka Haya:
Naona leo naulizwa sana nipo timu gani. Aisee mi ni simba till I die. Sijawahigi kuwa shabiki wa mpira kivileeee ila marehemu babangu alikuwa ni shabiki wa Simba kindaki ndaki. So toka nipo mdogo nashangilia simba. Yani ilikuwa simba wakishinda babangu anakodi pick-up zinabeba watu watu na mziki wanazunguka kuanzia mtaani kwenu enzi hizo mtaa wa kitomondo Temeke.Inazunguka Mtoni kwa Aziz Ally kote kule. Haha. Siku hiyo mpaka nilikuwa naruhusiwa kutoka getini kucheza na watoto barabarani.
Oh yeah, nimezaliwa Temeke mie. Nimekuja kuhamia Mbezi Beach in 1989, nna miaka 9.
Yani Simba kwangu ni kama CCM. Babangu kwa wanaojua alikuwa mkandarasi so kazi zoote alikuwa anafanya na serikali, babangu ndo aliejenga VETA ya Mtwara na barabara nyingi za mikoani kajenga yeye. Mawaziri wooote nilikuwa nawaita Uncle flani, Uncle flani. Kipindi cha uchaguzi nyumbani kulikuwa hakuna gari hata moja, zote zinaenda kwenye kampeni. Babangu alikuwa ni CCM kindaki ndaki. Yani angekuwa hai kipindi kile namchamba Magu nahisi angesaidiana na Magu jinsi ya kunikamata ila babangu angemwambia nikifikishwa Dar amkabidhi yeye. Haki babangu angenifungia chumbani mpaka akili zirudi sawa. Babangu angehisi ni chips mcDonalds zimeharibu akili 🤣🤣.
Yani hata ile kuchoma kadi ya CCM in 2017 ilikuwa ngumu mnooo kwangu. Maana CCM ndo ilikuwa kila kitu home kwetu. Na hata babangu angekuwa hai I think ningefanya nilichofanya. Ila laana za Mzee Kimambi zingenihusu. Mamangu ndo mpaka aligombeaga udiwani Tandika huko kupita CCM. Yani alikuwa wale wamama wa CCM kindaki ndaki. Yani wazazi wangu wangekuwa hai kipindi kile nafanya wanajeshi nchi nzima wako barabarani na vifaru vya nchi vinazunguka kila sehemu haki wazazi wangu wangekuja marekani kunikamata wenyewe wanikabidhi kwa Magu ila wangemwambia asiniue ila anifunge mpaka nipate adabu.
Post a Comment