HAJI Manara, Ofisa Habari wa Simba amesema kuwa hakuwa na namna ya kufanya zaidi ya kutimiza ahadi ambayo alitoa kwa shabiki wa Yanga, Omary Haji Mpili, maarufu kama Mzee Mpili.
Manara aliahidi kumpa mkwanja ambao ni milioni moja ikiwa Yanga ingeshinda mbele ya Simba, Julai 3.
Kilichotokea ubao wa Uwanja wa Mkapa baada ya dk 90, ulisoma Simba 0-1 Yanga jambo lililomfanya Mzee Mpili kuomba apewe pesa yake kwa kuwa hakuomba ila Manara yeye mwenyewe alisema kuwa atampa.
Jana, Julai 7, Manara alitimiza ahadi hiyo kwa kumpa Mzee Mpili milioni moja pamoja na maziwa tukio ambalo lilikuwa mubashara kupitia mitandao yake ya kijamii na kwenye chanel yake ya Manara TV kwenye youtube ameipandisha kazi hiyo.
Manara amesema kuwa mpira sio uadui bali ni urafiki na mambo ambayo huwa yanatokea nje ya uwanja hasa wanapokutana watani wa jadi ni furaha tupu.
"Ninaamini kwamba mpira sio uadui ila ni burudani kwa kuwa niliahidi basi lazima nitimize. Kwa hili hakika Mzee Mpili Kigoma utakwenda tena na ndege nitaongea na viongozi wa Yanga kwani kwa hamasa ambayo umefanya hustahili kupanda daladala," .
Kwa upande wa Mzee Mpili aliweka wazi kwamba mpira sio uadui huku akimuombea kheri Manara na familia yake wapate baraka kwa Mungu.
Post a Comment