Mambo 10 nilioyaona Simba vs Yanga Baada ya Mnyama Kumpiga Yanga


From @alikamwe Mambo 10 nilioyaona Simba vs Yanga

1: AND THE WINNER IS 🦁..KIGOMA IS REEED 🔴 MACHAMPION wa Nchi wamerejesha Heshima yao kwenye siku ya Heshima🙌 Well Done Simba SC

2: 'Turning Point' ya mechi ni Red Card ya Mukoko Tomombe. Kwa mchezaji wa aina yake.. kwa Uzoefu na umuhimu wake kwenye kikosi cha Yanga, ilikuwa ni zaidi ya utoto kwa alichokifanya. Ni kosa lililokwenda kuwatesa Yanga uwanjani na kuwaumiza mashabiki moyoni

3: 'Pitch' ya Lake Tanganyika kwa kiasi kikubwa ilipunguza 'quality' ya mchezo. Mpira ulichezwa kwa kubutuliwa sana! Angalau Didier Da Rosa alikuja na 'Game Plan' iliyoonyesha amedhamiria kupambana na changamoto ya kiwanja. Kivipi?

4: Kuanza na 'Dabo Straika' na kumuweka Bwalya mbele ya Taddeo Lwanga kuliwafanya washambulie kwa 'Second Balls'. Bocco na Mugalu walidondosha mipira mingi kwa Miquissone.. Game Plan hii ilionekana kuwapa tabu sana mabeki wa Yanga

5: Kocha wa Yanga, Nabi alistick ya System yake ya 4-2-3-1 Lakini ufanisi wa viungo wake ulipotea katikati ya kiwanja kutokana na changamoto ya Pitch. Huduma hazikwenda kwa kutosha pembeni ya kiwanja walipotega mitego yao

6: Luis Miquissone.. Happy Birthday Konde Boy🙌 Mchezaji mkubwa kwenye matukio makubwa. Katika kila kiwanja, dhidi ya viatu vya mabeki katili.. KONDE BOY ATAKUPA JASHO LAKE KWA ASILIMIA 100% .. WHAT A PLAYER

7: Well Play Bakari Mwamnyeto👏 Alijitahidi kupambana hewani. Akawa bora pia kwenye kuipanga safu yake ya ulinzi. Hata Yanga ilipocheza pungufu bado alijitahidi kuwa bora kuipush Timu icheze bila presha

8: Farouk Shikhalo🙌 MOJA YA MECHI nzuri sana kuicheza Tangu atue Yanga. Alikuwa bora kwenye kusoma hatari nyingi zilizoingia kwenye boksi yake

9: Lwanga.. Amewapa Simba kitu walichokikosa kwenye Derby iliyopita..'Spirit ya kiume kwenye kazi ya Kiume.🙌 Alipambana sana kupunguza movement za FeiToto na kuanzisha mashambulizi ya haraka kwa pasi ndefu

10: Presha ya Mechi ilikuwa kubwa kwa mwamuzi Ahmed Arajiga. Alichukua muda kiasi kuwa boss wa mchezo. Matukio mengi alishindwa kuyaamua mwanzoni kwa presha

Nb: Mzee Mpili Akalime sasa 😂


0 Comments

Post a Comment

Post a Comment (0)

Previous Post Next Post