Kutokea Nchini Kenya Kuhusiana na KIFO cha Polisi..Inawezekana Aliuawa na Kushikishwa Bastola

 


Askari Polisi wa Kenya Caroline Kagongo ambaye amekuwa akisakwa kwa wiki mbili kwa tuhuma za kuua Watu wawili wanaodaiwa kuwa Wapenzi wake wa zamani, amekutwa amefariki nyumbani kwa Wazazi wake huko Rift Valley.


Polisi wanasema Caroline alimpiga risasi mwenzake John Ogweno kisha akatorokea eneo la Juja Nairobi ambako nako alimuua Mwanaume mwingine aitwae Peter Ndwiga kwa kumpiga risasi chumbani hotelini.


Ripoti zinasema Caroline amejiua kwa kujipiga risasi akiwa bafuni kwa kutumia bastola ambayo alikuwa amejihami nayo na anayoshukiwa kuitumia kutekeleza muaji hapo awali.

Nafasi za Ajira Serikalini Bonyeza HAPA

Nafasi za Scholarships Bonyeza HAPA

Nafasi za Internships Bonyeza HAPA

Baadhi ya Watu mitandaoni nchini Kenya na maeneo mengine wamewaomba Polisi kufanya uchunguzi zaidi kuhusu chanzo cha kifo cha Polisi mwenzao huyo huku wakidai upo uwezekano kuwa aliuawa na kisha akashikishwa bastola mkononi.


Bado hadi sasa haijaewekwa wazi ukweli wa mfululizo wa matukio anayodaiwa kuyafanya, tunaendelea kufatilia



0 Comments

Post a Comment

Post a Comment (0)

Previous Post Next Post