Kumekucha..Simba Wamtangaza Mrithi wa Haji Manara..Huyu Hapa


Club ya Simba imemteua Ezekiel Kimwaga kuwa Kaimu Mkuu wa Idara ya Habari na Mawasiliano ya Klabu hiyo kwa kipindi cha miezi miwili baada ya Hajis Manara kuondoka Simba na kuachia nafasi hiyo.

Katika kipindi hicho cha miezi miwili Kamwaga atashiriki katika maboresho ya muundo wa utendaji wa Idara hiyo akiwa ni Mwandishi wa Habari mwenye uzoefu wa zaidi ya miaka 15 kwenye tasnia ya habari akifanya kazi katika Vyombo vya Habari vya ndani na Kimataifa.

Taarifa ya Simba SC imesema Kamwaga anaijua vizuri Club ya Simba na historia yake kwani amewahi kuitumikia katika nafasi za Msemaji wa Klabu na Kaimu Katibu Mkuu wa Simba.


0 Comments

Post a Comment

Post a Comment (0)

Previous Post Next Post