Kumekucha..Basata Watengua Maamuzi ya Miss Tanzania Kutompeleka Rosey Manfere Miss World




Baraza la Sanaa la Taifa - BASATA limesema halijaridhia na halijakubaliana na maamuzi ya kumuengua Miss Tanzania 2020/21 Rose Manfere kwenye ushiriki wa shindano la Dunia (Miss World 2021) mpaka pale Kamati ya Miss Tanzania itakapotoa sababu za msingi na kuzithibitisha.


Aidha BASATA limeilekeza kampuni ya "The Look" ambao ni waandaaji wa shindano la Miss Tanzania kuwasilisha jina la Miss Tanzania 2020/21 (Rose Manfere) katika shindano la Urembo la Dunia (Miss World 2021) Hii imekuja kufuatia Kamati ya mashindano ya Miss Tanzania kutangaza kumuengua Miss Tanzania 2020/21 kwenye mashindano ya Urembo ya dunia na nafasi yake kuchukuliwa na mshindi wa pili, Juliana Lugumisa.




0 Comments

Post a Comment

Post a Comment (0)

Previous Post Next Post