Kimenuka.. Shigongo Amuomba Rais Kumuondoa DED wa Buchosa



Mbunge wa Jimbo la Buchosa Eric Shigongo, amemuomba Rais Samia Suluhu Hassan, kuwahamisha Mkurugenzi wa Halmashauri ya Buchosa pamoja na Idara ya uhasibu katika Halmashauri hiyo, akiwatuhumu kwamba wamekuwa wakiibia fedha halmashauri hiyo.


Kauli hiyo ameitoa hii leo Julai 17, 2021, mkoani Dar es Salaam ambapo amesema kuwa Rais Samia amekuwa akijitahidi kupeleka fedha vijijini lakini utekelezaji wake umekuwa ni hafifu, kwa kuwa viongozi wengi wa Halmashauri wanaiba fedha hizo.



“Mimi nilikuwa sijawahi kuhitilafiana na Mkurugenzi wangu hata mara moja mpaka nilipoanza kufuatilia mapato ya ndani, mimi naomba Mheshimiwa Rais aniondolee Mkurugenzi, aniondolee idara ya uhasibu isipokuwa amuache Mwekahazina peke yake," amesema Mbunge Shigongo.



Aidha, Shigongo ameongeza kuwa, "Ninaomba Halmashauri ya Buchosa ikaguliwe sababu pesa zinapotea, fedha zinaliwa, mtu anakuja pale anafanya kazi miezi miwili tayari ana nyumba mbili wakati kipato chake hakitoshi kujenga nyumba mbili, kwa niaba ya watu wa Buchosa nasema jambo hili hatulikubali niungwe mkono ama nisiungwe mkono na Madiwani mimi nitasimama imara kuhakikisha fedha zinzokuja zinatumika vizuri".


0 Comments

Post a Comment

Post a Comment (0)

Previous Post Next Post