Kesi ya Sabaya na wenzake yapigwa kalenda




Mahakama ya Hakimu Mkazi Arusha yaahirisha kesi ya aliyekuwa mkuu wa Wilaya ya Hai, Lengai Ole Sabaya na walinzi wake 5 hadi Julai 16 mwaka huu watakapo fikishwa mashahidi wa upande wa Jamhuri kuwasilisha ushahidi dhidi ya kesi inayo wakabili.



 Lengai Ole Sabaya (34) na wenzake watano wanakabiliwa na mashtaka sita yakiwemo mawili ya ujambazi wa kutumia silaha.Leo Julai 2,2021 katika mahakama hiyo ilidaiwa mashtaka mengine manne yanayowakabili upelelezi wake bado haujakamilika.

Wakili wa Serikali, Tarsila Garvas aliomba kupangwa siku nyingine ili mashahidi hao waanze kutoa ushahidi wao na hakimu mkazi mkuu, Salome Mshasha alikubali maombi hayo na kuahirisha kesi hiyo hadi Julai 16, 2021.




0 Comments

Post a Comment

Post a Comment (0)

Previous Post Next Post