Supastaa Alikiba ambaye kwasasa anafanya vizuri kupitia kazi zake mbili alizoziachia mfululizo ambazo ni Ndombolo na #Salute, ameweka wazi kuwa suala la yeye kununua VIEWS YouTube katu hawezi kulifanya.
"Siwezi kujitekenya na kucheka mwenyewe" - ametweet @officialalikiba
Kiba amelijibu hilo akimpa ufafanuzi shabiki mmoja kupitia ukurasa wake wa twitter ambaye alihoji kuwa eti mkali huyo ananunua VIEWS.
Suala la views kwa wasanii limekuwa pasua kichwa kila uchao kwani shutuma za ununuzi wa VIEWS sasa ni endelevu baina ya wasanii kwa wasanii sambamba na mashabiki kwa wasanii wao.
Post a Comment