Kamanda Muliro Ang’aka Ataja Wanaopaswa Kumiliki Bastola

 


 Kamanda wa polisi Kanda Maalum ya Dar es Salaam, Muliro Jumanne amesema kuwa sio sifa kumiliki silaha endapo huna vigezo vya kuimiliki kwa kufuata sheria.

Akizungumza na waandishi wa habari leo Julai 19, 2021 amesema kumiliki silaha kuna sheria zake  na endapo ukizikiuka,  hatua za kisheria zitachukuliwa ikiwamo kifungo cha miezi 12 au faini ya Sh1 milioni au vyote kwa pamoja.

Amesema kuwa sheria inamtaka mtu aliyepewa silaha awe nayo muda wote kwani wakati mwingine kuiacha nyumbani au kwenye gari ni tatizo kulina na sheria ya umiliki wa silaha hiyo.


Similar News:

 Job Opportunity at Prime Minister’s Office, Procurement Officer



Aidha ametaja makundi yanayopaswa kumiliki silaha au bastola kuwa ni pamoja na kuwa Mtanzania, mwanadiplomasia, mtu wa kampuni ya ulinzi, au mtu mwingine yeyote lakini mwenye akili timamu



0 Comments

Post a Comment

Post a Comment (0)

Previous Post Next Post