Kama Movie.. Meneja asimulia Mwanzo Mwisho Tukio la Mauaji Sinza "Alimfumua Ubongo Mwenzake”




MENEJA WA Baa ya Lemax, Godlisten Augustine, amesimulia tukio la mauaji ya watu wawili yaliyotokea katika baa hiyo, jioni ya jana Jumamosi, tarehe 18 Julai 2021, akidai kwamba muuaji alikuwa analipa kisasi. Anaripoti Regina Mkonde, Dar es Salaam…(endelea).

Tukio hilo lilitokea jana baada ya Alex Koroso, maarufu kama Simba, kufyatua risasi ovyo kisha kuumua mtu mmoja aliyefahamika kwa jina la Gift. Baada ya kutekeleza tukio hilo, Simba alijiua kwa kujipiga risasi maeneo ya shingoni.

Akisimulia mkasa huo, Augustine amedai Simba alifika katika baa hiyo akiwa na jazba kuhusu tuhuma alizokuwa amepewa za kutishia watu kwa bastola na kushindwa kulipa bili ya vinywaji alivyokuwa anakunywa.

Amedai kuwa, muuaji huyo alifika katika baa hiyo, mwezi mmoja tangu alipokata mguu baada ya wenzake kumcheka, kutokana na kushindwa kulipa bili ya vinywaji alivyokuwa anaagiza “Simba ni mpita njia kwetu, kwa hapa anakuja siku moja moja. Tangu amelipa deni ilikuwa kama mwezi mmoja ndio akaja hapa.”


Meneja huyo wa baa amedai kuwa, Simba alifika katika maeneo hayo majira ya saa nne asubuhi huku akiwa amelewa.“yule bwana alionesha kama mtu amekesha kwenye pombe, alivyoamka akaja hapa na ile pombe aliyopewa hapa ikamrudishia kwenye motion kwamba ni mtu aliyelewa .”

Akielezea namna mauaji hayo yalivyofanyika, Augustino amedai kuwa, Simba aliamuru redio zizimwe baada ya hapo akaanza kufyatua risasi juu na moja wapo kumpata Gift.

“Baada ya dakika tano, Simba akaja akasema hapa kuna afisa usalama, zima redio. Mziki ulivyozimwa akapiga risasi juu, yule Gift na watu wengine wakanyanyuka na kuanza kusambaratika. Akampiga Gift risasi ya mguu, wakati anaendelea kukimbia akampiga tumboni. Gift akaanguka,” amedai Augustino.


Augustino amedai kuwa, baada ya kuona tukio hilo na Gift kupigwa risasi ya tumbo, aliamua kuwafungia ndani wateja na wahudumu wa baa hiyo, huku Simba akiendelea kurusha risasi hadi zilipoisha.

Amedai, zilipoisha aliongeza nyingine na kummalizia Gift kwa kumpiga risasi ya kichwa, iliyofumua ubongo wake.“Gift alikuwa bado hajafa ndiyo maana nikawa naangalia mtu kaenda wapi ili niweze kutoa msaada kumpeleka hospitali.”

“Lakini ikashindikana sababu alikuwa anapiga mtaa mzima, risasi ya tatu ikamalizia uhai wake. Alimpiga kichwani ikatokea kwenye ubongo,” amedai Augustino.

Augustino amedai kuwa, baada ya Simba kumuuwa Gift, alikaa katika kiti kisha akajipiga risasi kwenye shingo “alivyookaa kwenye kiti akajishuti, nikasema kajiua. Niliona amefanya kwenye shingo ikatokea juu. Kafa lakini watu wengi kinachowauma roho ni kumuua yule bwana pasipo kosa lolote.”


Inadaiwa kuwa, chanzo cha tukio hilo mgogoro kati ya Simba na baa hiyo kutokana na tabia yake ya kutolipa bili za vinywaji ambapo alikuwa ana deni la 677,000, pamoja na kuwatishia wengine kwa silaha.

Augustino amedai, kutokana na tabia yake ya kutolipa bili zake, mke wake ambaye hakumtaja jina aliamua kulipa fedha hizo na kusababisha baadhi ya watu waliomfahamu Simba kuanza kumtania mitandaoni.

“Alikuwa hataki kuingia kwenye baa sababu alidaiwa bili mpaka mke wake akaja kulipa, kwa hiyo watu wengine kwenye mtandao wakawa wanamtania kwa nini unakunywa pombe, mpaka ulipiwe. Kwa nini unakunywa bia unasumbua unalipa unavyojisiskia. Basi akawa na kinyongo,” amedai Augustino.

Augustine amedai, Simba alikuwa ni mtu wa fujo, mkorofi na mara kadhaa alikuwa anawatishia watu kwa bastola, hali iliyowakwaza watu na kusababisha walimripoti katika Kituo cha Polisi cha Mabatini.

“Mnamo saa 4.00 asubuhi mtu ahuyo ambaye amejipiga risasi, alifika eneo la baa. Alikuwa amepaki gari nje, alikuwa anaongea na watu tofauti wengine kwa furaha, wengine kwa jazba kama kawaida yake mtu wa fujo, kujisifia anapenda kujisisfu,” amedai Augustine.

Augustine amesimulia “nilipokutana naye akaniambia vipi bwana, nasikia mlienda kunishtaki Mabatini kwamba mimi nimewatishia watu na silaha katika baa ya kwenu. Nikamwambia hapana, hakuna mtu aliyeenda kukushtaki ni uchonganishi.”

Augustino amedai, baada ya kutoa maelezo hayo, Simba alimtaka amuite kiongozi wa baa hiyo, iliakazungumza naye.

“Akaniambia nipe niongee naye, wakaongea sikujua walichoongea ni nini, baada ya hapo akanirudishia simu yangu akasema anakuja hapa, nikaendelea na huduma. Baadae boss akaja, alivyokuja kakaa takribani dakika tatu,” amedai Augustine.


0 Comments

Post a Comment

Post a Comment (0)

Previous Post Next Post