Mwanamume mmoja wa Austria alielezea mshangao aliopata alipong’atwa na nyoka yenye urefu wa mita 1.6 kutoka katika choo chake.
Walter Erhart, 65, anasema kwamba aliona kitu kama nyoka baada ya kung’atwa. Nyoka huyo alitoroka kutoka kwa jirani yake anayefuga nyoka wengine 10 .
‘’Nilienda katika chumba changu cha kulala, nikawasha taa kama kawaida na kuketi katika choo na ghafla bin vuu nikahisi kitu kimening’ata’’.
Inadaiwa kwamba nyoka huyo alitoroka na kujificha katika bomba la maji taka kabla ya kuingia katika choo hicho. Akielezea , Walter alisema kwamba hatua hiyo ilisababisha uchafu katika kiti cha choo hicho.
‘’Niliona damu ikimwagika , hapo ndiposa niligundua nyoka alikuwa amening’ata’’. Alipoulizwa iwapo alimuona nyoka huyo kabla, Walter alijibu: Hapana, Niligundua tu nilipohisi kung’atwa.
Mtaalamu wa Wanyama Warner Stagl alisema kwamba baada ya kisa hicho alienda kuchunguza kuchunguza ndani ya bomba hilo la maji taka.
Mmiliki wa nyoka huyo amekuwa akifuga nyoka 11 katika nyumba yake ambayo ipo jirani na ile ya Walter na huenda akakabiliwa na mashtaka.
Post a Comment