Geita: Auawa baada ya kumfumania mama yake mzazi na mwanaume mwingine




JESHI la Polisi Mkoa wa Geita linawashikilia watu watano kwa tuhuma za mauaji ya kumchinja Budagala Vita (26), kwa kumcharanga kwa mapanga shingoni na kufariki dunia baada ya kumkuta mama yake mzazi akifanya mapenzi na mwanamume mwingine.

Akizungumza na waandishi wa habari jana, Kamanda wa Polisi wa mkoa huo, Henry Mwaibambe, alisema tukio hilo limetokea Juni 28, mwaka huu katika Kijiji cha Bokondo, Tarafa ya Butundwe, Wilaya ya Geita.

Kamanda Mwaibambe alisema, Budagala aliuawa kwa kukatwa na mapanga shingoni na watu wasiojulikana baada ya kumkuta mama yake mzazi akifanya mapenzi na mwanamume mwingine, wakati baba yake mzazi akiwa safarini mkoani Kagera.

Alisema kiini cha tukio hilo ni mgogoro wa kifamilia, baada ya baba wa marehemu, Vita Bupilipili, kusafiri kwenda kutafuta maisha Juni 26, mwaka huu na kumuacha mke wake pamoja na mtoto wake huyo.


 
Alisema Budagala alimkuta mama yake mzazi akifanya mapenzi na mwanamume mwingine nyumbani kwao na kusababisha mgogoro ndani ya familia hiyo.


0 Comments

Post a Comment

Post a Comment (0)

Previous Post Next Post