Mamlaka nchini Uingereza imeonya dhidi ya mikusanyiko mikubwa ya watu kabla ya fainali ya kombe la Ulaya EURO 2020 katika uwanja wa Wembley nchini humo hii leo kwa hofu ya kuenea aina mpya ya kirusi cha Delta kinachoambukiza kwa haraka.
Mamlaka hiyo ina wasiwasi hasa kuhusu athari za mikusanyiko mikubwa ya watu katika maeneo ya burudani na vilabu kote nchini humo watakaokuwa wakitazama mchuano wa timu ya taifa hilo iliyofika fainali kwa mara ya kwanza katika muda wa zaidi ya karne moja dhidi ya Italia.
Naibu kamishna wa polisi katika eneo hilo Laurence Taylor, amesema kuwa Uingereza bado iko katika mzozo wa afya ya umma.
London leo itakuwa mwenyeji wa mashabiki elfu 65, huu ukiwa mkusanyiko mkubwa zaidi katika uwanja wa Wembley tangu kuzuka kwa janga la virusi vya corona.
Post a Comment