Edo Kumwembe "Yanga Wahuni Sana Wameenda Kucheza Wakijua Thamani ya Derby"


Reposted from @edokumwembe Yanga 'wahuni'...inaanzia kwa mashabiki kwanza...unashangaa wakati ukiona kama vile hawako sawa na zimebaki siku chache wacheze na Mnyama wanakwambia 'Tunawachinja Wale'...unajiuliza kiburi wanakitoa wapi? Baada ya hapo wanajiambukiza kujiamini, mwishowe inafika na kwa wachezaji...Simba huwa wanakwama hapo. Wao wanategemea uwezo wao tu na wanakwenda na matokeo mfukoni, kuanzia mashabiki, viongozi hadi wachezaji. Yanga wanajikuta wakikimbia mara mbili ya uwezo wao. Bahati nzuri pia wamepata kocha ambaye anajua kuwapanga kwa discipline pale nyuma. Anatengeneza blocks mbili za haraka wakati timu haina mpira. Hapo hapo amegundua siri ya kumtumia Feisal kwa mbele, halafu Gift na Mukoko kwa nyuma. Hapo hapo wanashambulia kwa wingi wakiwa na mpira. Haishangazi kuona Gift alijikuta pale ingawa ni defensive midfielder.

Zamani angekuwa nyuma kuleeee. Simba huwa wanahitaji kupewa nafasi sana ya kucheza ili washine, Yanga huwa hawawapi hiyo nafasi. Wanawin kila second ball, wanaziba gaps kwa haraka na uzuri wa kocha wao Nabi ni kwamba wanaweza pia kutulia na mpira wakiwa na mpira. Kifupi Yanga wanakwenda kucheza Derby hiwakijua thamani ya Derby....wanapambana hasa, Simba wao huwa wanakwenda na matokeo mkononi huku wakijivunia matokeo yaliyotokea Champions League Afrika ambayo kiukweli hayana uhusiano na Derby. Ni kitu ambacho hata rafiki yangu Haji alikibeba kukipeleka katika press conference. Sometimes vipaji haviamui Derby...


0 Comments

Post a Comment

Post a Comment (0)

Previous Post Next Post