Diamond Platnumz Mali Anazotambia Akizigeuza FURSA Atakuwa Bilionea wa Kwanza Kijana Afrika



Na Andrew Chale(MNGONI ORG)

Msanii wa muziki wa kizazi kipya Naseeb Abdul aka Diamond Platnumz ambaye kwa sasa amekuwa akizidi idadi kubwa ya mashabiki amekuwa ndo msanii anayezungumziwa kila kukicha kufuatia kupost vitu vya kifahari.

Msanii Diamond amekuwa akipost magari na majumba pamoja na vitu vya thamani kama saa, cheni, mikufu, meno ya madini na mambo mengine ikiwemo pesa za kigeni.

Katika makala haya ya kiuchumi imemwangazia Diamond kama endapo atageuza mali hizo ambazo anatumia kutambia kuwa fursa basi ndie atakayekuja kuwa msanii wa kwanza bara la afrika kuwa tajiri.

Mbaki na dili na mikataba ya matangazo makubwa na madogo anayopata na kuendelea kupata, takwimu zinaonesha Diamond anaweza kuendelea kuwa maarufu zaidi miaka mingi inayo kutokana na namna anavyokabiariana na hali ya soko lake la muziki.

Amekuwa akiangalia jinsi gani ya kutoka kwenye 'game' na jinsi gani mashabiki wake watapokea ujio wake.

Hasi sasa kupitia mtandao wake wa kijamii wa Instagram, ameweza kufukisha idadi ya wafuasi waliomfuata yaani (followers ) 12.7Milioni.

Wafuasi hao ni mtaji tosha pja kuelekea ubiliobea kwa kugeuza ngebe na majigambo ya mali zake kuwa fursa.

Tukiacha mbali huko nyuma aliweza kuwa na bidhaa kama Chibu pafyumu pia Diamond Karanga na mengine mengi msanii huyu anaingiza pesa kupitia albam zake ambazo zinauzwa na kuona duniani lote kupitia mitandao ya kijamii ambayo inamuingizia pesa ndefu kama Youtube.

Pia ana bidhaa kama Wasafi tv, Wasafi radio, Zoom Xtra ambayo inadili na films na mambo ya muziki production kupitia miziki yake na ya wasanii wake wa kundi la WCB Wasafi.

Mnamo majira ya mchana 14 Julai msanii huyo ameweza kuonesha gari la ndoto yake linalosemekana lina thamani ya Ths. Bilioni 1.5 aina ya Roll Royce Cullinan 2021 rangi ya bluu 0 kilometa kama wanavyosema watoto wa mjini.

Kwa hatua hii kila mtu anapongeza a tuangalie na upande wa pili je anafanya haya kwa manufaa ya nani? Ili Forbes Afrika wamuone kama msanii mwenye ukwasi kwa Afrika ama anafanya haya ilikila mtu ajue kama anaingiza mkwanja mnono? .

Kila mmoja anamaoni yake ila mimi kama mwandishi wa makala hii naangalia upande wa fursa atakayoipata Diamond kupitia magari ya kifahari aliyonayo endapo atafuata ushauri wangu hapa JF.

Anamagari karibu aina zote ya kifahari namshauri asitumie tu muda wa kuonesha watu wanaomchukia ama anaoshindana nao kimuziki zaidi atumie fursa hiyo hiyo kuyageuza fursa hayo magari ilikuchochea uchumi wa Taifa.

Diamond anaweza kutengeneza mamilioni ya fedha haoa Tanzania na kuwa msanii pekee Afrika mwenye fedha nyingi endapo atatumia fursa hiyo.

Miongoni mwa fursa hizo ni pamoja na kuyatumia magari yake ya kufahari kuyaingiza barabarani na kuyakodisha kwa shughuli za kujipatia kipato ikiwemo harusi ama shughuli za kuigizia filamu ama matukio makubwa ya wageni wa kitaifa na kimataifa wanaweza kuyatumia hayo magari na kuingiza kipato.

Tanzania kwa wiki kuna shughuli za harusi zaidi ya 100 kwa mwezi? Nadhanu pesa nyingi anaweza kuingiza Diamond kupitia hayo magari yake.

Kuna viongozi na watu maalum wanaweza kuja Tanzania na magari ya kuwapakia yakatumika haya ya Diamond endpao tu ataamua kuyageuza katika fursa za kibiashara.

Kupitia andilo hili namuona Diamond akielekea kuwa Bilionea kwa kugeukia fursa kwa kila kitu alichonacho baada ya kuwa vya kuonesha kama mapambo au maigizo sasa aelekee kwenye fursa ya kichumi. Hakika atatoa ajira kwa vijana wengi na kuacha kukaa vijiweni.

Kupitia vitu alivyonavyo pia anayo nafasi ya kufungua jumba maalum la makumbusho na kuweka vitu vyake humo watu wakawa wanatoka maeneo mbalimbali kufika kujionea vitu hivyo ambapo anaweza kuingiza kiasi kikubwa cha fedha kwa muda mrefu zaidi kama wafanyavyo wafu wengine wakiwemo wasanii na watu maarufu.

Kama gari moja kati ya mbili za Escalade alizonazo Diamond akaamua kuziingiza sokoni kisha akanunua Noah mayai ama Halfad kwa ajir ya kufanyia shughuli za shuttle tour kwa maana 'Diamond Shuttle tour VIP' basi nina hakika anaweza kuingizia wazo lake fedha nyingi zaidi kwa muda wote na fedha zake zikarudi maradufu.


 

Nafasi za Ajira Serikalini Bonyeza HAPA

Nafasi za Scholarships Bonyeza HAPA


Anaweza kununua gari hizo za Halfadi ama coastal zaidi ya 20 na akaziweka majiji makubwa tu zikafanya kazi maalum pesa atakazoingiza ni kunwa kuliko kuwa na magari ambayo anaishia kupiga nayo picha na kutukana watu kisa tu walimkandia kuwa hatoweza miliki hayo magari.

Nina hakika Diamond atapata ujumbe popote alipo atasikia andiko hili ambalo naamini ni la kiuchumi lenye kuchochea maendeleo.



0 Comments

Post a Comment

Post a Comment (0)

Previous Post Next Post