Diamond, Ali Kiba, Harmonize Kupewa Tuzo Wiki Hii




Dar es Salaam, Tanzania, Julai 13, 2021. Jumla ya wasanii tisa(9) wa Tanzania watapokea tuzo wiki hii kwa kuvunja rekodi ya kuwa na wasikilizaji wengi kupitia App ya Boomplay.


Tuzo hizo almaarufu ‘Boomplay Plaques’ hutolewa mara moja kila mwaka ili kutambua jitihada za wasanii wanaofanya vizuri kwenye App ya Boomplay.

 

Hiini mara ya pili kwa tuzo hizo kutolewa ambazo ni mahususi kwa wasanii ambao wameendelea kufanya vizuri kupitia kazi zao za muziki ndani ya mwaka mmoja uliopita.

 

Katika taarifa iliyotolewa kwa vyombo vya Habari, Meneja Mkuu wa Boomplay nchini Tanzania, Natasha Stambuli amesema, “Wasanii kama Diamond Platnumz, Alikiba, Harmonize, Rayvanny, Nandy, Mbosso, Zuchu,Aslay na Darassa ni baadhi ya wasanii ambao wameendelea kuvunja rekodi kupitia App ya Boomplay na nifuraha yetu kuwatambua na kuwapa tuzo.

 



Pamoja na mambo mengine ambayo tumeendelea kushirikiana na wasanii wetu, huu ni uthibitisho wa dhamira yetu endelevu ya kuhakikisha kuwa tasnia ya muziki inaendelea kukua na kusonga mbele,”

 

“Kama Kampuni inayoongoza kwenye utoaji wa huduma ya kusikiliza na kupakua muziki Afrika, Boomplay siku zote ipo mstari wa mbele katika kutambua wasanii waoendelea kufanya vizuri kwa kuvunja rekodi mbalimbali kupitia kazi zao za muziki.
Matarajio ya Kampuni ni kuona wasanii wengi zaidi wanapata tuzo hizi kila mwaka”.

 

Bi. Stambuli ameongeza kuwa vigezo vilivyotumika kuchagua wasanii ni pamoja na wingi wa usikilizwaji (streams) wa wimbo wa msanii husika, albamu na usikilizwaji unaotokana na ujumla wa nyimbo za msanii. Takwimu za washindi zimechukuliwa kuanzia mwezi Novemba 2020 hadi Mei 2021.





0 Comments

Post a Comment

Post a Comment (0)

Previous Post Next Post