Deus Kaseke Asaini Miaka Miwili Yanga




KATIKA kuhakikisha wanakiboresha kikosi chao kwa ajili ya msimu ujao, Yanga imemuongezea mkataba wa miaka miwili kiungo Deus Kaseke.

Huyo atakuwa mchezaji wa pili kuongezewa mkataba.

 

Kaseke ni kati ya wachezaji kipenzi cha Kocha Mkuu wa timu hiyo, Nasreddine Nabi ambaye tangu akabidhiwe kikosi hicho amekuwa akimtumia nyota huyo katika kikosi cha kwanza.

Huyo anakuwa mchezaji wa pili kuongezewa mkataba Yanga kati ya hao ambao mikataba imemalizika, mwingine ni Mapinduzi Balama.

 

Kwa mujibu wa taarifa ambazo imezipata Championi Ijumaa, Yanga hivi sasa inafanya usajili wake kwa usiri mkubwa na tayari imewaongezea mikataba wachezaji wake ambao Kocha Mkuu wa timu hiyo, Nasreddine Nabi amewapendekeza.

 

Mtoa taarifa huyo alisema kuwa kati ya wachezaji waliongezewa mikataba yupo Kaseke ambaye mkataba wake unamalizika mwishoni mwa msimu huu.Aliongeza kuwa tofauti na wachezaji wanaoongezewa mikataba, pia mabosi wa timu hiyo wanaendelea na usajili mpya wa kitaifa na kimataifa.

 

“Usajili wetu wa msimu huu, tumeupanga ufanyike kwa siri na hadi hivi sasa tumewasajili wachezaji wapya na waliomaliza mikataba wawili.“Usajili huo unafanywa kwa mujibu wa mapendekezo ya kocha wetu Nabi.“

 

Kikubwa tunataka kusuka kikosi kitakacholeta ushindani katika msimu wa ligi na michuano ya kimataifa. Kati ya wachezaji walioongezewa yupo Kaseke ambaye mara baada ya mechi dhidi ya Simba kumalizika, alisaini miaka miwili,”alisema mtoa taarifa huyo.

 

Alipotafutwa Kaseke kuzungumzia hilo alisema: “Mimi bado mchezaji wa Yanga kwa misimu mingine miwili baada mkataba niliokuwa nao awali kumalizika.




0 Comments

Post a Comment

Post a Comment (0)

Previous Post Next Post