Dereva amuua kondakta wakigombania abiria





Jeshi la Polisi Mkoa wa Dodoma linamshikilia Dereva wa Daladala (jina linahifadhiwa) kwa kosa la mauaji ya Kondakta wa daladala, Juma Hamisi (25) wakati wakigombea abiria.

Akizungumza na Waandishi wa Habari, leo Alhamisi Julai Mosi, 2021 Kamanda wa Polisi Mkoa wa Dodoma, Onesmo Lyanga amesema Mtuhumiwa alitenda kosa hilo Juni 15, 2021 katika Mtaa wa Mji Mpya jijini Dodoma ambapo alimuua kwa kumpiga na jiwe kichwani wakati wakigombea abiria katika eneo hilo.

Kamanda Lyanga amesema dereva huyo mara baada ya kumuona abiria walianza kumgombea na marehemu kila mmoja akitaka aingie katika gari yake.

Amesema mara baada ya msako Juni 19, mwaka huu wamefanikiwa kumkamata dereva huyo akiwa mafichoni katika Kijiji cha Galapo Wilaya ya Babati, Mkoa wa Manyara.


 
Kamanda Lyanga amesema mtuhumiwa anatarajia kufikishwa mahakamani kwa kosa la mauaji.


0 Comments

Post a Comment

Post a Comment (0)

Previous Post Next Post