CardiB na Rapa Offset Watuletea Habari ya Mtoto Mwingine


Familia ya wasanii wa muziki kutoka nchini Marekani inayowakutanisha Rapa Bercalis Almanzar #CardiB na Rapa Kiari Cephus #Offset inatarajia kuongeza member mwingine kwenye familia yao kati ya tarehe 13-15 mwezi wa 9 mwaka huu.

Taarifa ya tarehe hiyo imekuja baada ya kusogezwa mbele kwa kesi kati ya #CardiB anaye mtuhumu Tasha K ambae ni blogger maarufu nchini Marekani kuwa kamchafulia jina baada ya blogger huyo kutumia ukurasa wake wa YouTube kusema kuwa Rapa huyo anajiuza na kuwa tabia yake hiyo imemsababishia kupata ugonjwa aina ya Herpes.

Kesi kati ya wawili hao ilikuwa isikilizwe tarehe 13 mwezi wa 9, lakini mwanasheria wa #CardiB, Lisa F. Moore ameomba isogezwe mbele hadi miezi miwili ijayo kwa kuwa mteja wake anatarajia kujifungua katika kipindi hiko hiko.

Taarifa za ujauzito wa pili wa #CardiB ziliwekwa wazi na yeye mwenyewe alipoonekana akiperform na kundi la Migos kwenye tuzo za BET za mwaka huu.




0 Comments

Post a Comment

Post a Comment (0)

Previous Post Next Post