Cardi B Amekanusha Taarifa za Kwamba Menejimenti yake iliwahi Kuwa na Mkakati wa Kumpoteza Nicki Minaj


Cardi B amekanusha taarifa za kwamba Menejimenti yake iliwahi kuwa na mkakati wa kumpoteza Nicki Minaj kwenye muziki. Madai hayo yalitolewa na Mwanadada Jessie Woo ambaye alifanya mahojiano na Hollywood Unlocked.

Jessie alisema mwaka 2017 alikutana na mmoja kati ya watu kwenye menejimenti ya Cardi B na alimwambia kuhusu mpango huo "Tunataka kumleta Cardi B kwenye muziki, hivyo lengo letu ni kumuondoa Nicki Minaj." ilikaririwa kauli hiyo. Sasa Cardi B ambaye kwa sasa ni mjamzito ameibuka na kulisemea hilo, kupitia comment yake ambayo aliiacha kwenye ukurasa wa The Neighborhood Talk, Cardi alisema hakuna ukweli wa hilo.

"Ni uwongo, nachukua kuja kuelezea upuuzi ambao hauna maana. Jessie Woo ndiye yule msichana ambaye aliwahi kunifata DM akiniomba ushauri kwa sababu alikuwa amesaini na label yangu ya zamani na akawa anahisi kama aliyekuwa meneja wangu anamtaka. Kama mtu amewahi kukwambia kitu kuhusu kumshusha mwanamke mwenzio, kwanini ulisaini naye? Kingine ni kwamba najua hawezi kusema kitu kama hicho." aliandika Cardi B.

Ujio wa Cardi B kwenye muziki ulileta uhasama mkubwa kati yake na Nicki Minaj lakini tayari wamemaliza tofauti zao.




0 Comments

Post a Comment

Post a Comment (0)

Previous Post Next Post