Serikali ya Tanzania, imepokea zaidi ya dozi milioni moja za chanjo ya Covid-19 kutoka nchini Marekani, kupitia Mpango wa Usambazaji Chanjo wa Covax kwa uratibu wa Umoja wa Afrika (AU).
Chanjo hiyo imepokelewa na Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Dk. Doroth Gwajima na Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kikanda, Balozi Liberata Mulamula katika Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere jijini Dar es Salaam.
Kwa upande wake, Balozi wa Marekani nchini, Donald Wright kupitia akaunti ya ubalozi wa Marekani Twitter, amesema kuwasili kwa chanjo hiyo ni kielelezo cha uimara wa ubia wetu wa miaka 60 na dhamira yetu ya dhati kwa Tanzania.
Post a Comment