Breaking News: Anna Mghwira Afariki Dunia

 


Arusha. Aliyekuwa Mkuu wa Mkoa wa Kilimanjaro, Anna Mghwira amefariki dunia leo Alhamisi Julai 22, 2021 katika Hospitali ya Mount Meru mkoani Arusha alikokuwa akipatiwa matibabu

Mdogo wa Anna Mghwira na marafiki zake wa karibu wamethibitisha kutokea kwa kifo hicho leo

"Ni kweli Mghwira amefariki mchana huu, alikuwa amezidiwa akawa amepelekwa chumba cha wagonjwa mahututi (ICU)," amesema mdogo wake.

Zaidi ya wiki moja iliyopita alikuwa amelazwa katika Hospitali ya Nkoaranga kwa tatizo la kupumua ambapo baadaye hali yake kuwa mbaya alihamishiwa hospitali ya Mount Meru.



0 Comments

Post a Comment

Post a Comment (0)

Previous Post Next Post