Bilionea Jeff Bezos Ang’atuka Amazon




BILIONEA namba mbili duniani, mwanzilishi na mmiliki wa Kampuni ya Amazon, Jeff Bezos on leo Jumatatu, Julai 5, 2021, atakabidhi kiti chake cha u-CEO wa Kampuni hizo kwa Andy Jassy, baada ya kuiongoza kampuni hiyo kwa miongo miwili huku akipata mafanikio makubwa katika mapinduzi ya teknolojia ya kuuza vitabu hadi kufikia mauzo ya dola trilioni 1.75 na vitu mbalimbali mtandaoni.

 

Kampuni hiyo ilitangaza Mwezi Februari kuwa, Bezos atastaafu kazi ya u-CEO ambapo alikuwa mtendaji mkuu wa kampuni hiyo na sasa atabaklia Mwenyekiti Mtendaji ili apate muda zaidi wa kutazama biashara zake nyingine kama  Washington Post, Blue Origin na taasisi zake za kijamii.

 

Licha ya kukabidhi mikoba ya majukumu yake kwa Andy, Bezos atabakia kuwa mshauri mkuu wa kampuni hiyo kwa miaka kadhaa ijayo na kiongozi mkuu wa bodi ya wakurugenzi kwa kuuwa pia ndiye mmiliki mwenye hisa nyingi zaidi katika kampuni hiyo kubwa duniani.

 

Jeff anang’atuka ikiwa ni miezi michache baada ya kampuni yake kutengeneza faida kubwa ambayo haijawahi kutokea na kumfanya utajiri wake kuongezeka na kufikia dola bilioni 186 huku akipanda chati ya mabilionea wakubwa duniani, biashara ambayo aliifanya wakati wa janga la corona.

 

 

Mpaka mwezi uliopita, Bezos alikuwa akimiliki hisa kiasi cha milioni 51.2 sawa na takribani asilimia10 ya Amazon akifuatiwa na Kampuni ya Vanguard Group, inayomiliki asilimia 6.5 ya Amazon

 

Bezos ataendelea kumsaidia polepole CEO mpya Jassy kwa muda mpaka atakapokwiva kuiendesha kampuni hiyo. Wawili hao wamefanya kazi pamoja tangu siku za mwanzo wakati kampuni hiyo ilipoanzishwa iaka ya 2000.


0 Comments

Post a Comment

Post a Comment (0)

Previous Post Next Post