Bilionea Amfanyia Kufuru Fei Toto





BILIONEA na Mdhamini wa Yanga, Gharib Mohammed, amemfanyia kufuru kiungo wa timu hiyo, Feisal Salum ‘Fei Toto’ kwa kumzawadia gari jipya aina ya Toyota Crown sambamba kuboresha mshahara wake.

 

Kiungo huyo ambaye kipenzi cha Wanayanga, katika msimu huu amekuwa katika kiwango kikubwa huku akiaminika na kila kocha anayekuja kikosini hapo akimpa nafasi ya kucheza kikosi cha kwanza.

 

Kwa mujibu wa taarifa ambazo imezipata Spoti Xtra, Fei Toto alipewa gari hilo siku moja mara baada ya mchezo wa Kariakoo Dabi dhidi ya Simba uliopigwa wiki moja iliyopita kwenye Uwanja wa Mkapa, Dar es Salaam uliomalizika kwa Yanga kushinda bao 1-0 lililofungwa na Zawadi Mauya.



Mtoa taarifa huyo alisema kuwa, bilionea huyo amempa gari hilo baada ya kiwango kikubwa alichokionesha kwa kumiliki safu ya kiungo.

 

Aliongeza kuwa, kabla ya gari hilo kupewa, hivi karibuni alimboreshea mshahara wake kutoka Sh 2Mil na kufikia Sh 5.5Mil ambao anaupata sasa hivi.

 

“Hivi sasa Fei Toto anaishi maisha ya tofauti na awali kwani hivi karibuni ameboreshewa mshahara wake ambao ni mnono.“

 

Pia mara baada ya mchezo wa Kariakoo Dabi dhidi ya Simba alipewa gari jipya aina ya Toyota Crown rangi nyeusi.

 

“Gari hiyo amepewa na GSM baada ya kuonesha kiwango kizuri katika dabi hiyo baada ya kuwapoteza viungo wa Simba,” alisema mtoa taarifa huyo.Kupitia akaunti yake ya Instagram, Fei Toto ametupia picha akiwa juu ya gari hilo akionekana kufurahia maisha.

STORI NA WILBERT MOLANDI, Dar



0 Comments

Post a Comment

Post a Comment (0)

Previous Post Next Post