Barbara Awachimba Mkwara Mzito Yanga





Mtendaji Mkuu (C.E.O) wa Simba, Barbara Gonzalez.

WAKATI wakiwa wanatarajia kukutana kwenye fainali ya Kombe la Shirikisho (FA), Mtendaji Mkuu (C.E.O) wa Simba, Barbara Gonzalez ni kama ametuma ujumbe mzito kwa wapinzani wao Yanga kwa kubainisha wazi kwamba watachukua ubingwa huo.

 

Mtendaji huyo ameongeza kwamba licha ya ugumu wa kukabiliana na watani zao hao lakini mipango yao ni kulibeba taji hilo sambamba na ubingwa wa ligi kuu.



Simba na Yanga zote zimepenya fainali ya FA baada ya kushinda mechi zao za nusu fainali kwa bao 1-0 kila moja, Simba wakishinda mbele ya Azam FC na Yanga wakiwachapa Biashara United.

 

Barbara amesema kwamba licha ya ugumu ambao wanao wapinzani wao wote kwenye ligi lakini hesabu zao ni kuhakikisha kuwa wanachukua mataji hayo mawili mwisho wa msimu.

 

“Mashabiki wetu tunawaomba watuombee hasa kwenye mechi hizo mbili, ya ligi na FA. Mechi zote ni ngumu kwa sababu hakuna timu rahisi kwenye ligi kuu lakini tuko tayari kupambana, tulisema mwanzo wa msimu kwamba tunahitaji vikombe vyote kwenye FA na ligi kuu.”

Stori na Said Ally,Dar es Salaam



0 Comments

Post a Comment

Post a Comment (0)

Previous Post Next Post