Afia Gesti kwa Kunywa Vidonge vya Kuongeza Nguvu za Kiume




MWANAUME mmoja aliyejulikana kwa jina la Fredrick Opiyo mwenye umri wa miaka 50 amekutwa amefariki dunia katika nyumba ya kulala wageni ya Rurago kaunti ya Muranga nchini Kenya huku kifo chake kikileta utata.

 

Ripoti ya polisi imesema kuwa huenda jamaa huyo alimeza vidonge vya kuongeza nguvu za kiume kupita kiasi. Mlinzi wa gesti hiyo alitoa taarifa katika Kituo cha Polisi cha Maragua baada ya mpenzi wa jamaa huyo waliyekuwa naye kumfahamisha kuhusu kifo cha mwanaume aliyekuwa naye chumbani.

 

Mary Mwende alisema mpenzi wake Fredrick Opiyo alikuwa amekodi chumba cha kulala majira ya saa tatu usiku, naye mwanadada huyo aliwasili majira ya saa nne usiku, siku ya Jumatatu, Julai 26, 2021.

 

Kabla ya wawili hao kulala, Mwende alisema walienda kutafuta chakula cha jioni, walikula ugali na samaki na mpenzi wake hakuonyesha dalili za kuwa mgonjwa.

 

“Jamaa huyo baadaye aliingia bafuni akaoga, alimweleza mpenzi wake waingie kitandani walale lakini naye alitaka kuoga. Alipoondoka kwenye bafuni, alimkuta marehemu akiwa amelala kwenye kitanda akiwa na matatizo ya kupumua, dakika chache baadaye alikata roho,” ripoti ya polisi ilieleza.

 

Katika uchunguzi, Polisi walikutwa mipira tatu ya kondomu, moja ikiwa imetumika na miligramu 100 ya viagra (dawa za kuongeza nguvu za kiume) kwenye chumba hicho.

 

Ofisa Mkuu wa Muranga Kusini alifika eneo la tukio na kumuru mwili wa marehemu kuchukuliwa na kupelekwa katika chumba cha kuhifadhia maiti katika hospitali ya Murang’a Level 5 ambapo umehifadhiwa. Hata hivyo, uchunguzi zaidi unafanya kubaini zaidi chanzo cha kifo chake.



0 Comments

Post a Comment

Post a Comment (0)

Previous Post Next Post