KIKOSI cha Yanga leo Juni 23 kimekwea pipa kuelekea Tabora ambapo kitakuwa na mchezo wa Kombe la Shirikisho dhidi ya Biashara United.
Mchezo huo unatarajiwa kuchezwa Uwanja wa Al Hassan Mwinyi, Juni 25.
Huu ni mchezo wa hatua ya nusu fainali ambapo mshindi atakutana na mshindi wa mchezo kati ya Azam FC v Simba utakaochezwa Uwanja wa Majimaji, Juni 26.
Kwa mujibu wa Ofisa Habari wa Yanga, Hassan Bumbuli amesema kuwa wapo tayari kwa ajili ya mchezo huo na wanahitaji kufanya vizuri.
"Tupo tayari kwa ajili ya mechi zetu ambazo zimebaki na kikubwa ni kuona kwamba tunapata ushindi ndani ya uwanja.
"Wachezaji wapo tayari na kila mmoja anahitaji kuona kwamba tunapata matokeo chanya," .
Post a Comment