Ni headlines za mastaa wawili wa kike hapa nchini Wema Sepetu "Tanzanian Sweetheart" na Hamisa Mobetto ambao wameonekana kuvaa vazi la aina moja kwenye mitupio yao na hata pozi kufanana katika picha walizopiga.
Katika mavazi yao wameonekana wote wamevaa nguo nyeupe juu mpaka chini na kutupia kofia inayojulikana kwa jina la kibandiko kwenye vichwa vyao.
Wa kwanza kuvaa vazi la aina hiyo ni Wema Sepetu ambapo alitokelezea nalo kwenye siku ya Uzinduzi wa Album ya Zuchu iliyofanyika siku ya Julai 18 iliyofanyika Mlimani City Dar es Salaam.
Baada ya kumalizika kwa shughuli hiyo Wema Sepetu akapost picha akiwa na vazi hilo na akaandika "Malkia wa usiku wa mwisho, kubali au kataa ndio iko hivyo, nilijua kuwaka jana aisee niligiwa simu mpaka na watu wasiojulikana mkisikia nimetekwa msiogope, nimeona nijisifie maana kama kunijaza mmenijaza wenyewe"
Sasa leo Juni 20, 2021 Hamisa Mobetto naye akatupia tena vazi la aina kama hiyo na picha zake ameshea kwenye page yake ya Instagram kwa kuandika "Kuwa na ujasiri au italiki, kamwe usiwe wa kawaida".
Kiukweli 'Diva's' wote hawa wamependeza sana kwenye mitupio hiyo ila unaweza ukashea comment yako kwamba nani katupia zaidi.
Post a Comment