Waziri Dkt. Damas Ndumbaro Amtimua Kazi Meneja

 


Waziri wa Maliasili na Utalii, Dkt. Damas Ndumbaro amemsimamisha kazi Meneja wa Shamba la hifadhi ya Misitu la Silayo lililopo Bukombe Mkoani Geita kwa tuhuma za kuhamisha wananchi katika maeneo yao kinyume na taratibu.

Akizungumza na waandishi wa Habari amesema tayari amemuagiza katibau mkuu Wizara ya Maliasili na utalii kumsimamisha Meneja huyo ambapo ameunda timu ya uchunguzi aliyoipa muda wa wiki mbili

Dkt. Ndumbaro amemsimamisha kazi kutokana na kuwepo kwa malalamiko kuwa meneja huyo amefanya operashioni ya kuwaondoa watu bila kuwa na kibali maalumu kutoka wizarani.

Serikali imesitisha mabadiliko ya mitaala mipya ya masomo

” Ndugu wanahabari tumewaita hapa kutolea ufafanuzi juu ya malalamiko yaliyotolewa na Mbunge wa Jimbo la Bukombe,Mh. Dotto Biteko kuhusu Meneja wetu huyo kufanya operesheni ambayo imewasababishia uharibifu na hasara wananchi wa maeneo hayo.

”Hivyo kufuatia malalamiko hayo tunamsimamisha kazi Meneja wa Msitu huo, Thadeus Shirima kupisha uchunguzi wa tuhuma zinazomkabili, na nimuagize Katibu Mkuu kupeleka Meneja mwingine,” Amesema Dkt Ndumbaro



0 Comments

Post a Comment

Post a Comment (0)

Previous Post Next Post